Michezo
Jerry Muro ateuliwa kuwa msemaji mpya wa Yanga
Mtangazaji wa zamani wa vituo vya ITV na TBC1, Jerry Muro ameteuliwa kuwa msemaji mpya wa club ya Yanga.
Jerry Muro
Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, Muro anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto ambaye sasa atakuwa meneja wa timu hiyo. Gazeti hilo limedai kuwa uamuzi huo wa Yanga ulitolewa katika kikao kilichofanyika Jumapili hii.
Chanzo kimoja kimeliambia gazeti hilo kuwa mkataba wa Kizuguto ulikuwa unakwenda ukingoni na hivyo wameamua kutomwongezea mkataba.