Habari

Jela miaka 30 kwa kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili

Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu imemhukumu Seleman Emanuel (21) mkazi wa Kijiji cha Sayusayu wilayani humo kwenda jela miaka 30 baada ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha pili na kumsababishia ujauzito.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Fredrick Lukuna alitoa hukumu hiyo Ijumaa hii baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka bila kuacha shaka.

Aidha Hakimu huyo alisema kuwa anatoa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya ya kutaka kutenda kosa kama hilo katika jamii.

Mwendesha Mashitaka aliieleza Mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alishirikiana kimwili na mwanafunzi huyo kike mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Isanga na kumsababishia ujauzito.

Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Nassibu Swedy alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mwezi Julai mwaka jana .

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents