Burudani

Je wajua somo ambalo halifundishwi shuleni na vyuoni lakini lilipaswa kufundishwa?

Tunapokuwa mashuleni tunafundishwa vitu vingi sana lakini kuna baadhi ya mambo hutafundishwa ila utasikia yakitajwa mara chache sana na hivyo kuonekana kama hayana umuhimu mkubwa.

Labda inawezekana ni shule niliyosoma au chuo nilichosoma kikawa tofauti na kile ambacho mwenzangu umekisoma. Je ulishawahi kuwaza na kufikiri, ni wangapi walishaweza kufundishwa mambo ya fedha na hasa kusisitiza kuhusu akiba?

Labda kwa wale ambao wanasoma masomo ya biashara na uchumi labda limegusiwa lakini waliosoma masomo mengine hilo jambo haufundishwi na kuaminika kwamba kila mtu anatakiwa kujua. Lakini kwa ukweli wa maisha mambo hayako hivyo kabisa watu wengi hatujui somo hilo inavyopasa na hivyo hatulichukulii uzito unaohitajika.

Kuweka akiba kwa wakati ujao kama umesoma kwa mkopo utagundua kitu hiki kwamba hela ikiingia matumizi yanakuwa makubwa na zikiisha watu wanaanza kula mikate na chai na wakati mwingine kuvusha kabisa yaani unakunywa chai asubuhi na mchana unaacha ipite halafu unakuja kula usiku.

Hii yote ni kwasababu hatukujengwa kwenye msingi wa kuweka akiba kwaajili ya nyakati zijazo ndio maana kuna wakati wanafunzi wanakuwa na hela na wakati mwingine hela wanakuwa hawana. Si kwamba hela hawakupata bali hawakuweka akiba au kupiga mahesabu ya siku watakazokaa hapo chuoni.

Hela ya kutumia wakati wa dharura. Wanafunzi wengi hatutengi hela ya dharura tunatafuta kujionyesha  na fahari ya maisha ukiwa chuoni wakati inawezekana kabisa ukaweza kuweka akiba kama ukiamua kutoka chuoni na mwisho wa siku ukatoka na kitu. Ukiweza kufanya hivyo utaweza kupata hela ya dharura ambayo inakusaidia mbele ya safari yako ya masomo na siku za usoni. Wengi wanasema haiwezekani lakini ukiwa na akili nzuri ya kuwaza na kuweza kuondoa matumizi yasiyo ya lazima.

Watu wengi hawakumbuki kuwa wakitoka chuo au wakimaliza kuna muda mrefu watapoteza kabla ya kupata kazi Ikiwa kama ulipata mkopo wa asilimia 100% inamaanisha hauna tatizo katika masomo yako, na nilishawahi kukutana na tatizo la mwanafunzi ambaye alikuwa anazunguka kutafuta msaada kutoka chuo fulani na baada ya utafiti tukagundua anapata mkopo asilimia 100% ingawa ulikuwa hautoshi ada ya chuo hicho bali alikuwa anapata fedha ya vitabu na matumizi mengine ya kuchapa masomo hayo na kutoa kopi ambayo angeweza kuitunza ili kufidia pale ambapo ada inakuwa haitoshei.

Lakini alikuwa anatafuta maisha ya kifahari ya yeye kuwa na muziki mkubwa chumbani kwake n.k. Hii yote inahitaji kutumia akili na inahitaji vile vile watu wafundishwe ili kupata ukweli huu, si kwamba wote wanaujua bali elimu inahitajika katika eneo hili.

Kuna watu wakiweza kuweka akiba kuanzia mwaka wa kwanza wanaweza kutoka na mtaji. Huhitaji mamilioni kujua nini cha kufanya, bali unahitaji kuwa na akili timamu ujue kitu gani unatakiwa kufanya.

Ni bahati kupata mkopo ambao huhitaji kuweka rehani kitu chochote zaidi ya kudhibitisha uraia wako. Je unataka kuanzisha biashara mara tu utakapo maliza chuo? ukishindwa kufikiri wakati unaanza ni ngumu kufikiri wakati umemaliza chuo na huku huna hata uhakika wa kula au kulipa kodi ya chumba. hebu fikiri kwamba unaingia chuo na unaweza kuweka akiba ya shilingi 500/- kila siku katika lile bumu la chakula baada ya miaka miwili utakuwa na shilingi ngapi? Wavivu wa mabadiliko watasema hicho kitu hakiwezekani abadani, lakini inawezekana ukiamua ni kwamba tu hatujajengwa kwenye utamaduni huo.

Hivi kwanini huwa hatujiulizi watu wengi wakistafishwa ghafla wengi hufa? Wengine hawafi ila wanateseka na msongo wa mawazo ambao unajiuliza kwani kumetokea nini? Mwandishi mmoja alisema ukishindwa kuweka mipango unakuwa umepanga moja kwa moja kufeli. Kwa sababu hiyo hakuna mpango mkakati wa kuweka akiba ya kukusaidia kuishi baada ya kustaafu ndicho hicho hicho kinachotutesa hata tukiwa vyuoni tunatumia vyote tunavyopata bila kufikiri kesho itakuwaje au nikitoka hapa naenda kufanya nini nisipopata kazi mapema?

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents