Habari

Je wajua madhara ya kuchanganya pombe na dawa aina ya Metronidazole (Flagyl)

Metronidazole (Flagyl) ni dawa ya antibaotiki (antibiotic) inayotumika kutibu aina tofauti za bacteria (bacteria) na vimelea (parasites) mbalimbali vya magonjwa.

Na hutolewa ikiwa katika mfumo wa vidonge vya kumeza au vidonge maalumu ambavyo huwekwe kwenye uke (vaginal suppository) na wakati mwingine hupatikana kama krimu ya kujipaka kwenye ngozi (topical cream)

Kutumia/ kunywa pombe wakati unatumia dozi ya metronidazole (FLAGYL) ni hatari kwa afya yako, kwani vitu hivi viwili huchanganyika na kuleta athari inayojulikana kitaalam kama Disulfiram like effects.

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea pindi utakapotumia vitu hivi viwili kwa pamoja;
• Kuumwa na kichwa (headaches)
• Kushindwa kupumua (breathlessness)
• Kizunguzungu (dizziness)
• Kichefuchefu na kutapika (nausea and vomiting )
• Kuongezeka au mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (increased or irregular heartbeat)
• Matatizo ya ini na figo
• Joto na kujaa (severe flushing)

Kitaalam mtu anatakiwa ajitahidi kuepuka kunywa pombe pindi anapotumia dawa hivi na kujitahidi kutokunywa pombe masaa 72 (siku 3) baada ya kumaliza dozi kwani dawa hizi hutumia masaa 48 kuondolewa (cleared) ndani ya mwili wa binadamu.

Kipindi hiki pia ni kizuri kujizuia kutumia dawa za kikohozi na mafua (cough and cold remedies) na kusafishia kinywa (mouthwashes) kwani zina kiasi Fulani cha pombe (alcohol). Tafuta ushauri wa mtaalam wako wa afya kama hauna uhakika na hali yako ya kiafya.

Your Health, My Concern

BY FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher
Pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]
[email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents