Habari

Je wajua kwanini kila unachokionja baada ya kupiga mswaki huwa na ladha mbaya

Toka ukiwa mdogo mpaka unazeeka umekuwa ukijiuliza kwanini kila kitu unachokula au kukionja huwa kinakuwa na ladha mbaya mara tu baada ya kusafisha kinywa chako kwa kutumia mswaki ulioweka dawa ya meno.

Dawa nyingi za mswaki huwa zinakemikali zifuatazo Sodium lauryl sulfate, sodium laureth sulfate (SLS) and sodium lauryl ether sulfate (SLES) ambazo hupunguza nguvu ya ukinzani ili kutengeneza povu (foaming action) kwenye dawa ya meno ili kusaidia katika kuondoa mabaki ya vyakula kwenye kinywa chako.

Lakini pia kemikali hizi hukinzana na utendaji kazi wa taste buds (huhusika na utambuzi wa ladha) kwa kuvunja vunja phospholipids kwenye ulimi wako. Matokeo yake husababisha ladha ya uchachu (bitter tastes) nahii ndo sababu kila unachokionja na kukila huonekana kibaya mara baada ya kusafisha meno yako.

Lakini hali hii huondoka mara tu baada ya mda mfupi. Niwatoe hofu watumiaji wa dawa za meno kuwa hali hii ya kuhisi uchachu haina madhara yeyote kiafya.

Your Health, Our Concern

Imeandaliwa na;
FORD A. CHISANZA
Scientist/Researcher/pharmacist
Location: Off Mandela Road, Mabibo – External,
P.o.Box: 77150, Dar Es Salaam, Tanzania.
Mobile:+255 652466430/+255 684363584
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents