Habari

Je unaishije hapa mjini kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi?

Inawezekana unaanza kujiuliza, naishi vipi kwa namna gani? Maisha thamani yake iko kwenye uhai, ambacho inamaanisha kuishi bila uhai huo hakuna maisha tena.

blackvoters-blackcandidates

Hivyo tunapoelekea kwenye kipindi hiki nyeti kila mmoja ana jambo lake na anajaribu kutafuta faida yake mwenyewe kulingana na eneo alilopo. Mwenzangu na mimi inawezekana upo upo na unajiingiza kwenye mijadala kichwa kichwa bila kupima na kujua hawa watu ulionao au wanaokuzunguka wako kwenye mlengo upi na wana madhumuni gani?

Ukiwa na akili timamu, tafuta usalama wako kwanza kabla ya kuongea au kujiingiza kwenye mijadala husika. Hakuna mtu ambaye anaweza kukwambia ukweli ila maisha haya yana thamani ya kuishi kuliko yakikatizwa bila sababu. Katika kauli na mazungumzo yako unatakiwa kujua unaongea kwa niaba ya nani au kumnufaisha nani? Na kama uko mtaani unaongea na nani? Je unajua wanaweza kufanya nini ili kukuhakikishia sauti zao zinasikika?

Wanasiasa wao huweza kupambana kwa maneno na mwisho wa siku na wanaweza kukaa meza moja na wewe unabaki ukishangaa hiki ni nini? Unatakiwa kuwa na akili ya ziada hasa linapokuja suala la usalama wako binafsi na mahusiano ya ndugu zako jamaa na marafiki, usije ukaharibu familia yako au ukapoteza marafiki kwa sababu tu ya msimamo wako wa kisiasa. Kitu ambacho unajua ni kwamba kwa gharama yoyote ile wanaofaidika ni wachache kuliko walio wengi bali hutumia watu kama mimi na wewe wanaoweza kuhatarisha maisha yao binafsi bila kugusa familia zao kwasababu wanajua mchezo huo.

Ni mimi na wewe tu ambao tunafikiri tunasaidia kumbe tunatumiwa bila ya kujua, kila kitu ambacho unakifanya katika kipindi hicha cha kuelekea uchaguzi unatakiwa kuwa makini kwani tatizo likikukuta linabaki kwako wewe na familia yako tu. Wanasiasa wao watakuwa na maisha yao huko yakiendelea. Wasikilize kwa umakini mkubwa chukua tahadhari inapobidi halafu fanya maamuzi mwenyewe, usitafute watu kwasababu hujui wanatafuta nini na wamelipwa na nani kufanya hivyo wanavyofanya.

Ogopa kutumiwa na hao watu, angalia wewe na familia yako. Hii haimaanishi usipige kura, la hasha sikiliza sera zao na piga kura.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents