Habari

Je unafikishaje habari mbaya kwa bosi wako au mtu aliye juu yako?

Tunapoendelea kuiangalia taaluma na maisha ya huko makazini kuna vitu vingi ambavyo tunatakiwa kujifunza kila siku. Jambo la msingi la leo tunaangalia umuhimu wa namna ya kuwasilisha habari mbaya kwa bosi wako. Habari mbaya tunayoizungumzia hapa, inahusika moja kwa moja na biashara au utendaji makazini.

Office-worker-getting-shouted-at-2184349

Mfano watu wameshindwa kufikia malengo ya mauzo ambayo yaliwekwa kwa mwezi uliyopita, na bosi wenu wa juu anatakiwa kujua maendeleo yakoje?

 

Kama ilivyo mnapotoa bidhaa mpya bosi wenu anajua mapema iwezekanavyo hivyo hivyo hata habari mbaya za kushindwa kuuza nayo inatakiwa kumfikia haraka iwezekanavyo kabla hajaipata sehemu nyingine.

 

Usijidanganye kwamba vitu havitatokea au umezoea kuwarushia watu wengine lawama pale ambapo mambo mabaya yametokea na vitu vizuri vikitokea wewe kama mkuu wa idara unaponda kuonekana ni wewe umefanya.

 

Tunashoangalia hapa ni namna ya kufikisha habari bila kuharibu kazi yako au ya watu wengine, kwasababu mabosi wengi hawapendi habari mbaya au hawapendi kusikia vitu vimeshindikana au havikufanyika kama ilivyotarajiwa.

Kama una habari mbaya zifikishe kwa bosi wako, na hapa ni taratibu za msingi za kufanya unapofikisha habari hizo;

 

Hakikisha unachangua muda muafaka au muda sahihi na mahali sahihi. Usijaribu kuchelewesha habari na wakati huo hutakiwi kupeleka kiholela holela labda wakati anaongea na wateja au yuko kwenye lift na wewe unaanza kutoa maelezo. Omba kukutana naye ili aweze kukusikiliza na wewe uongee katika mazingira tulivu na bosi wako atajua kuwa jambo hilo ni la umuhimu mkubwa kwamba linahitaji muda muafaka au uliopangwa kwa ajili ya hilo tu.

Fanya Kazi yako. Kama kosa kubwa limefanywa ni kwenye nyaraka wakati wa utoaji wa ripoti bosi atataka kujua ni kwanini. Hivyo unashauriwa kukusanya habari za kutosha kujua kwanini mambo yalienda vibaya kabla ya kuongea na bosi wako.

Uwe Makini katika maongezi yako na ulenge kusudi la hayo maongezi na si vinginevyo

Bosi wako atataka kujua tatizo na madhara yake kibiashara. Epuka kurusha lawama kwa mtu fulani, ingawa inaweza kuonekana ni nzuri unaporushiwa wengine lawama. Zingatia tatizo na usiruhusu hasira zikuzinge bosi wako anapofoka. Kumbuka wewe ndio mtu ambaye unaweza kumhakikishia bosi wako matokeo ya tatizo na suluhisho la hilo tatizo na namna gani lisitokee tena.

Onyesha Ushirikano

Usipeleke tatizo halafu ukaachia hapo. Jiandae kuongea kitu kama , “Baada ya kuona hivi tulifanya hivi na hivi” halafu onyesha ufumbuzi unaowezekana kuhusu tatizo hilo. Elezea suluhisho hilo na namna litakavyoweza kusaidia na itachukua muda gani kutekeleza.

Maliza jambo hilo

Wewe kama mkuu wa idara unatakiwa kuomba msamaha kwa tatizo hilo kwa ufupi halafu elekea kwenye ufumbuzi wa tatizo.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents