Burudani

JCB makala aja na nakala za makala

Msanii kutoka kundi la watengwa la mjini Arusha amesema muda sio mrefu anadondosha albam yake akiwa nje yakundi baada ya wenzake wawili  (Chindo man na Yyuzo) kuwa nje ya nchi kwa muda mwingi. Albam hiyo yenyewe ina jumla ya nyimbo kumi na sita ambayo ameipa jina la nakala za makala.

Akiongea na bongo5 kutoka jijini Arusha JCB alisema ameshamaliza kila kitu na kilichobaki ni kudurufu tu nakala na kuziingiza mtaani. “nimeshamaliza kila kitu kinachohusu mastering na baada ya siku tatu naelekea jijini Dar es Salaam kudurufu na kiiachia album mtaani”

 

Akiiongelea album yake JCB alisema ni album bora katika album bora za hip hop kwani hata production yake imefanywa na watayarishaji tofaut tofauti wakiwemo watayarishaj wanaochipukia lakini wanaojua kile wanachokifanya

Kuhusu muelekeo wa muziki wa bongo JCB alikiri kuwa kweli muziki unakwenda mrama “muzki wetu kiukkweli umepoteza muelekeo mzuri japo wasanii tunajitahidi sana kuufikisha mahali pake ila bado serikali haijatuzingatia kvile.”
Aliendelea kusema JCB “mimi nahisi huu muziki utkaja kuwa ajirakubwa sana na ya kutegegemewa hapo baadae kwani nina imani hizi harakati kuna siku zitakaa sawa tu na watu watatambua mchango wa muziki katika hii jami”

Kwa upande mwingine JCB amewashangaa wasanii wanao endeleza bifu kwani anaamini bifu sio kitu kinachokuza muziki “wasanii wanaoendeleza bifu nawaona kama hawaja kua kwani katika kitu kinachoua muziki basin a bifu zisizo na mpango zipo, pia bifu zinakufanya uonekane sio mwema hata katika jamii. Wako wapi 2Pac na BIG?!” Alimalizia kwa kutola mfano huo.

JCB alaizitaja baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albam hiyo ni pamoja na Arusha, Kjiti, Moment of silence, Ninapo, Drive slow, Bongo flava part one na two, kijenge ya juu, Prison break, Usinitafute, Tumetoka mbali, na nyingine nyingi. Pia wasanii walioshiki ktika album hiyo ni pamoja na Chndo man, Kazz kutoka Nairobi Kenya, Chaba, Kamaa kutoka ukoo flani maumau, Ibra da hasla na wengine kibao tu.
JCB alimalizia kwa kusema  “WASANII TUWE NA UPENDO”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents