Burudani

JCB: Kufanya kazi na msanii wa Bongo Fleva si kitu kibaya

By  | 

Rapper JCB amewapa somo wasanii wa Hip Hop na wadau wengine wasiopenda kuona msanii wa muziki huo akiachia wimbo wa pamoja na msanii wa Bongo Fleva.

JCB amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM Alhamisi hii kuwa msanii wa Hip Hop akifanya kazi na msanii mwingine anayefanya muziki tofauti na huo haimaanishi ndio ameusaliti muziki huo.

“Kufanya Kazi na msanii wa Bongo Fleva haimaanishi umeisaliti Hip Hop,” amesema JCB.

Hivi karibuni msanii huyo anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina ‘Tumeula Gang’.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments