Burudani

J.C.B: Kuachia Sokoni Nakala za Makala

 

Msanii wa kizazi kipya Jacob Makalla a.k.a JCB baada ya kuwa kimya muda mrefu amerudi upya kwenye game la Hip Hop na kusema mashabiki wake wategemee makubwa na Mengi kutoka kwake.

Msanii huyo amejigamba kwa kuachia albam yenye jumla ya nyimbo 16 huku akielezea ukimya wake kuwa kujipanga upya na sasa amerudi madini ya ajabu. Kwa sasa nina mistari ya ajabu,wapinzani wake Mjifiche!’ Alisema msanii JCB.

JCB amezitaja baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Movement of silence,Kijiti,Kijenge ya juu,Usinitafute,Prison break,Ninapo,arusha na nyinginezo,anasema na kuongeza kuwa albamu hiyo imerekodiwa ndani ya studio za Watengwa chini ya prodyuza David Bakari a.k.a Daz.

JCB anayetokea pande za Arusha hususan kundi la Watengwa, alisema kuhusu kundi hilo kwamba,wamepunguza speed kwani baadhi ya wasanii hao wako safarini Sweden akiwemo Chindo man.

Aliongezea kwamba hakuna kitu kilicho haribika kwani ni muda mfupi watakuwa wameshatimba Arusha na hapo ndipo wataanza kuachia vitu vile vilivyo sababishsha tukawa kimya.

JCB amebainisha kuwa albamu hiyo iliyojaa kila aina ya maudhui inauzwa buku kumi tu.Ukiitaka basi wasiliana nae kwa namba yake ya kiganjani

0713 641677 au 0784 641677

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents