MahojianoVideos

Video: JCB atimkia Ufaransa, lakini aacha ujumbe


Mwanamuziki wa Hip Hop kutokea jiji la Arusha, JCB, ambae aliwahi kuchukua tuzo ya wimbo bora wa Hip Hop kupitia wimbo wa Ukisikia Paah katika tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2011, amekwenda nchini Ufaransa kufanya kazi za kisanaa.

Kwa mujibu wa JCB mwenyewe ambaye Bongo5 ilipata nafasi ya kufanya nae interview siku kadhaa kabla ya kusafiri, alisema anakwenda huko kufanya mishe mishe kwa maana ya harakati mpya za kimuziki ambazo anategemea zitamletea mafanikio.

Aidha katika mahojiano ambayo bongo5.com imefanya nae (ambayo utayaona hapa chini) JCB ameongelea mengi ambayo anayaona yanazorotesha maendeleo ya muziki wa Hip Hop, kubwa zaidi akizitupia lawama vyombo vya habari upande wa maredio kwa kuwa nyimbo zao (wana Hip hop) hazipewi muda wa kutosha katika playlist za vipindi vyao.

Kwa sasa JCB yupo katika maandalizi ya Album huko Ufaransa akimshirikisha msanii mwingine wa Hip Hop Kindo Man ambaye anaishi Ufaransa.

Angalia Interview ya JCB hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents