Bongo Movie

JB awataka wasanii wa filamu kuacha kuwasema vibaya viongozi wao

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Jacob Stephan aka JB amewataka wasanii wa filamu kuacha mara moja kuwasema vibaya viongozi wao.
Jb

Akizungumza na Bongo5 leo, JB ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa Bongo Movie Unit, amesema haoni kama ni busara kukaa na kuanza kumsema vibaya kiongozi uliyemchagua mwenyewe ili akuongoze.

“Haya ni matatizo ya club na kuna watu ambao wanahusika kuzungumza kuhusu udhaifu wa uongozi, siyo kila mtu anaweza akaongea. Tunajua kila mtu anaweza kuongea lakini nawataka wasanii wenzangu kuwa wastarabu, na nachukua fursa hii kuwakanya watu ambao hawakupewa ruksa ya kuongea mambo ya bongo movie. Kwanini uongee bila kuteuliwa uongee? Watu wanavyoongea wanachochea ugomvi. Tatizo lililokuwepo kwa wasanii wanataka kila mtu aongee. Hata kama kuna matatizo lazima kuwe na mazungumzo ya ndani ili kumaliza tofauti zilizopo,”alisema JB.

Katika hatua nyingine JB amezungumzia uwezo alioonesha Q Chillah katika filamu yake mpya ya Hukumu ya Ndoa Yangu.

“Q Chillah kacheza kama kijana Mkenya aliyekuja kuharibu ndoa ya watu. Q Chillah ana uwezo mkubwa sana kabla Q Chillah hajaanza kuwa mwanamuziki alikuwa anaigiza katika kundi ambalo lilikuwa linaongozwa na King Master. Kwahiyo nilikaa na director marehemu Adam akasema huyu anaweza kucheza hii nafasi na kweli amefanya vizuri sana. Watu waitafute hiyo filamu waone.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents