Burudani

Jay Z awa rapper wa kwanza kupata heshima hii

Jay Z ametengeneza rekodi yake kubwa duniani kwa kuwa rapper wa kwanza kuchaguliwa kwenye tuzo za heshima duniani kama ‘Songwriters Hall Of Fame’.

Rapper huyo amechaguliwa katika kipengele hicho pamoja na waandishi wengine akiwemo Kenneth Edmonds maarufu kwa jina la Babyface, Jimmy Jam & Terry Lewis, Robert Lamm, Max Martin, James Pankow na Peter Cetera.

Baada ya kuchaguliwa katika tuzo hizo, mtandao wa muziki wa Tidal kupitia mtandao wa Twitter umempongeza Jay kwa kuandika, “Congratulations to @S_C_, the first rapper to be inducted into the prestigious Songwriters Hall Of Fame.”

Naye Chance The Rapper amempongeza bosi huyo wa Tidal kwenye mtandao huo kwa kuandika, “S/o to my OGs, Jay Z and Jimmy Jam & Terry Lewis, who were elected to the Songwriters Hall of Fame today. I hope to one day make it there.”

Tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa Juni 15 mwaka huu katika hoteli ya Marriott Marquis iliyopo New York City.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents