Burudani

Ripoti: Tiwa Savage asainishwa na Roc Nation

Jay Z ameripotiwa kukubali kusainishwa kwa msanii wa Nigeria, Tiwa Savage kwenye label yake, Roc Nation.

Tiwa_Savage's_studio_portrait

Kwa mujibu wa ripoti ya Urban View ya Nigeria, Jay Z ameshawishiwa na uwezo wa Tiwa na alikubali kusainiwa kwake May 24. Imedaiwa kuwa deal lilisimamiwa na wawakilishiwa Roc Nation, Briant Biggs na Shawn Pecas.

Hafla rasmi ya kumtangaza kama mwana familia mpya wa Roc Nation haijafanyika na bado label hiyo haijathibitisha. Kama ni kweli, Tiwa atakuwa msanii wa kwanza kutoka Nigeria kusainishwa kwenye label hiyo na kujiunga na Rihanna, Big Sean, DJ Khaled na wengine.

Balozi huyo wa Forte Oil, MTN na Pepsi kwa sasa yupo chini ya label ya Don Jazzy, Mavin Records.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents