Burudani

Jay Moe apinga kumchana Izzo Bizness kwenye ‘Nisaidie Kushare’

Jay Moe amepinga kumchana Izzo Bizness kwenye wimbo wake mpya ‘Nisaidie Kushare’.

Tetesi hizo zimeibuka kutokana na Izzo kudaiwa kuwa ni miongoni mwa wasanii wanaoongoza kuomba kuwekewa matangazo yao mitandaoni. Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Jay amesema wimbo huo haujamgusa Izzo na wala hana bifu naye.

“Mimi sina bifu na Izzo Biznezz. Siwezi kumtungia nyimbo za kumchana. Mimi sijamlenga mtu mmoja kwenye wimbo wangu bali nimewachana wote wanaoandika nyimbo mbovu sana halafu anakutumia umsaidie kuweka kwenye mitandao hata mwezi mzima halafu wimbo ukija kuusikia unatamani kufuta picha,” amesema rapper huyo.

Kwa sasa wimbo huo umeonekana kufanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga japo unasiku chache tangu alipouachia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents