Burudani

Jason Derulo aishtumu American Airlines kwa ubaguzi

By  | 

Muimbaji wa muziki wa RnB wa Marekani, Jason Derulo amelishtumu shirika la ndege la American Airlines kutokana na ubaguzi wa rangi wakati alipokuwa akitokea Miami kwenda Los Angeles.

Chanzo kimoja kimedai kuwa baada ya kuonekana Derulo na watu wake wa karibu wangechukua muda mwingi wa ukaguzi wa mizigo yao walimwacha mtu mmoja ashughulikie hilo. Lakini pia imedaiwa kuwa mabegi matatu pekee ndio yalikaguliwa bure kati ya mabegi 19 ambayo aliyokuwa nayo rafiki wa Derulo.

Derulo amesema alikuwa kwenye ndege ndipo alipopigiwa simu na rafiki yake aliyemweleza kuwa American Airlines walitaka kumtoza $4,000 kwaajili ya mabegi hayo. Muimbaji huyo amesema baada ya kushuka kwenye ndege, yeye na washkaji zake walikutana na polisi 15 na muda huo mfanyakazi mwingine wa shirika hilo akaanza kuwatukana lakini walipogundua kuwa ni mtu maarufu walibadilisha lugha.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Derulo amethibitisha kutokea kwa ubaguzi huo kwa kuandika:

@americanair I spent millions on your airline throughout the past ten years between myself and my entire staff but have still experienced racial discrimination today at miami airport!!! Called 15 police officers on me as if I’m a criminal! It’s not ok that when you find out who I am the gears change! Fuck that!! I want answers #conciergekey #conciergekeymember #thecaptainneedstoshowrespecttoo cause he could #cashmeoutsidehowboutdat #notypo #ifiwasanyoneelseiwouldhavebeenarrested

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments