Michezo
James Rodriguez asainishwa na Real Madrid kwa dau la £60m
Real Madrid wamekubali kumsainisha mshindi wa kiatu cha dhahabu katika kombe la dunia lililomalizika hivi karibuni nchini Brazi, James Rodriguez kutoka Monaco.
Mchezaji huyo wa Colombia amesaini mkataba wa miaka sita na timu hiyo na alifanyiwa vipimo Jumanne hii.
Nipo sawa
Madrid imelipa dau la £60million, na kuufanya uhamisho wa Rodriguez kushika nafasi ya nne katika orodha ya uhamisho ghali zaidi kwenye historia ya soka baada ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.