Burudani

Jah Prayzah azidi kunogewa na Bongo Flava

By  | 

Ni dhahiri, Jah Prayzah amenogewa na ladha ya muziki wa Bongo Fleva.

Muimbaji huyo kutoka Zimbabwe, anamshukuru Diamond kila kukicha, ambaye alimshirikisha katika wimbo wake wa ‘Wotora Mari’ na kumpatia tobo kubwa Afrika kwa kuanza kusikilizwa zaidi maeneo mbalimbali Afrika, na kupelekea kujinyakulia tuzo ya Listener’s Choice Awards ya MTV MAMA mwaka jana.

Sasa mkali huyo ameonekana akiwa studio na msanii kutoka WCB, Harmonize na kuandika ujumbe katika mtandao wa Instagram unaoashiria maandalizi ya wimbo wao mpya.

“In the studio again with another Tanzanian big star @harmonize_tz .Zimbabwe neTanzania ?,” ameandika Jah katika mtandao huo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments