Burudani

Jaffarai kufungua gereji ya magari, azungumzia kurudi kwenye muziki

Rapper Jaffarai amezungumzia mipango yake ya kufungua gereji mpya ya magari pamoja na kuachia wimbo wake mpya mwaka huu.
DSC_0258
Jaffarai akiwa ndani ya ofisi ya Jaffarai Carwash

Jaffarai ameiambia Bongo5 kuwa Carwash yake imemfanya awe na mipango mipya wa kufungua tawi pamoja na kufungua gereji ambayo itakuwa ikishughulika na kila kitu kihusianacho na magari.

“Mimi niko poa kwa kila mtu sina tatizo na mtu ndio maana unawaona macelebrity wengi wanakuja kwenye Carwash yangu kirahisi kwa sababu mimi ni rafiki yao pia. Lipo wazo la kufungua tawi lakini nina wazo la kuongeza vifaa zaidi ili ofisi iweze kufanya kazi nyingi zaidi kwaajili ya magari. Lakini kikubwa zaidi nataka kufungua gereji kubwa zaidi ili kufanya vitu vingine vyote vya kuhusu gari,” alisema Jaffarai.

Kuhusu muziki, rapper huyo wa Wateule amesema mwaka huu atarejea tena.

“Pamoja nipo busy kwenye kazi zangu lakini bado narekodi at the same time. Nina nyimbo tayari ambazo nimeshazirekodi. Nafikiri baada ya hizi fiesta fiesta kabla mwaka huu haujaisha nitakuwa nimetoa ngoma. Mimi muziki naona upo poa tu kwa sababu mimi nina njia zangu. Mimi Naju nipite vipi ili niweze kurudi. Ni kujitambua tu kuangalia unataka uimbe nini na kwa wakati gani. Hicho ndo kitu kikubwa. Hata wasanii wengine wanafeli kutokana hawaangalii ‘nifanye nini na kwa wakati gani’.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents