Bongo Movie

Jacqueline Wolper hafikirii kufanya filamu mpya leo wala kesho

Mashabiki wa filamu za kibongo wataendelea kumkosa Jacqueline Wolper kwenye screen zao hasa kama wanataka kuona filamu zake mpya. Msanii huyo amesema hafikirii kurudi kwenye filamu kwa sasa kutokana na hali ya soko la filamu kuendelea kudorora.

Jacqueline Wolper (600x400)

Wolper Gambe ameiambia Bongo5 kuwa bado yupo yupo sana na filamu zinazoenekana kutoka sasa ni zile alizofanya kitambo.

“Sasa hivi hali bado sio nzuri katika mauzo ya filamu ndio maana nasema bado siwezi pata picha nitarudi lini kwenye filamu,” amesema. “Let’s say naingia mwezi wa tano lazima niangalie kazi ya mwezi wa pili, wa tatu na wanne. Kwahiyo nikiangalia kazi ya mwezi wa pili na wanne nitajua sasa naingia vipi. Nikisema sasa hivi nianze kuzungumza lini nitakuja na nimejipanga vipi, nitakuwa muongo. Sasa hivi bado hali sio nzuri ndio maana hunioni nikitoa filamu mpya,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents