Habari

Jacky Wolper aifurahia aka yake mpya ‘Wolper Gambe’

By  | 

Muigizaji mrembo wa filamu, Jacqueline Wolper amesema alifungua mwaka kwa kuongeza aka mpya, Wolper Gambe, jina analotaka liwe alama yake kwa kila kitu atakachofanya.

Jacqueline_Wolper

Hata hivyo amewaambia mashabiki wake kuwa jina hilo halitokani na unywaji pombe uliopitiza.

“Silewi na si mpenzi wa vileo lakini napenda muziki sana jina langu limetokana na muziki ambao naupenda sana ndio maana kwa sasa najiita Wolper Gambe, ukiniita Wolper Gambe umefurahisha nafsi yangu kiukweli, watu wanajua eti Gambe ni pombe hapana, hizo ni swaga tu za sisi vijana, kitu kingine ninachopenda ni kumiliki gari nzuri,” aliimbia Filamu Central.

Alipoulizwa kuhusu gharama ya gari yake mpya ya ‘Mini Cooper’, mrembo huyo alisema gari yake ni ya gharama kubwa lakini si rahisi kuitaja hadharani wakati kuna watu wana shida na hawawezi kumiliki hata fedha ya kununulia chakula.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments