Burudani

Izzo B kuachia ‘Ball Player’ ft. Ngwair & Quick Rocka Jumatano hii

izzo bbb

Jumatano hii mashabiki wa Izzo Bizness wategemee kitu kipya kutoka kwake. Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Simwinga anatarajia kauchia single yake mpya iitwayo ‘Ball Player’ aliowashirikisha Quick Rocka na Ngwair.

Izzo ameimbia Bongo5 kuwa beat ya Ball Player imetengenezwa na Nahreel huku vocal na final mixing ikafanywa na Lamar wa Fish Crub.

Amesema wazo la kuja na wimbo wenye jina la ‘Ball Player’ ni kulinganisha juhudi za mchezaji mpira awapo uwanjani ambaye huwa na pilila pilika muda wote na jinsi ya kutumia mfano huo katika maisha ya kawaida. Amejitolea mfano yeye wakati anakuja Dar es Salaam kutokea Mbeya alifikia kwa washkaji lakini kwa sasa anaishi kwake mwenyewe kutokana na juhudi zake katika kutafuta maisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents