Picha

Izzo B ashukuru kutimiza ndoto yake ya kumshirikisha Jay Mo

Kila msanii mkubwa amewahi kuwa na role model wake kabla ya kuupata ustaa. Huenda Juma Mchopanga aka Jay Mo alikuwa na influence kubwa kwa muziki wa Emmanuel Simwinga aka Izzo B kiasi ambacho hitmaker huyo wa Riz-One kufanya ngoma na mzee wa Kimya Kimya kimekuwa kama ndoto iliyotimia.

6f6009108bb611e2979f22000a1f8ae3_7

Jana Izzo alikuwa studio za MJ Records kufanya ngoma mpya aliomshirikisha Jay Mo na hakusita kushare furaha yake kwenye Instagram kwa kupost picha baada ya recording session.

“12/03/2013 nilifanikiwa kutimiza ndoto yangu kwa kuweza kurekodi na J MOE beat by KTB vocal na mixing by @masterjtz #Godzgood ,” ameandika Izzo.

Hivi karibuni Izzo alimshirikisha pia Ngwair kwenye wimbo wake Ball Player.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents