Burudani

Iyanya wa Nigeria adaiwa kudanganya kuwa amesaini dili ya ubalozi wa Lenovo

Mmoja kati ya wasanii wa Nigeria ambao wanakubalika sana kwa sasa nchini humo na Afrika, Iyanya hivi karibuni alitangaza kuwa amepata dili ya kuwa balozi wa Lenovo.

Iyanya lenovo

Kupitia Instagram hit maker huyo wa ‘Le Kwa Ukwu’ aliandika “New Product!!! New Ambassador!!! Brand Ambassador!!! Lenovo!!! Iyanya!!! Task Direct 2014 Started # Triplemg”.

Mbali na Iyanya kutoa taarifa hiyo, meneja wake aitwaye Ubi Franklin pia alithibitisha juu ya dili hiyo, “It’s true, it cost about N150 to N170 million and the duration is for 24 months”.

Mtandao wa Naija Ghists wa Nigeria umedai kuwa umefuatilia swala hilo kutaka kupata ukweli kwa kupiga simu makao makuu ya kampuni hiyo ya Lenovo, ambao walisema hawajui chochote juu ya taarifa hizo na kuwaelekeza kwa mwakilishi wa Lenovo wa Nigeria ambaye baada ya kupigiwa simu alidai kuwa hata Iyanya hamfahamu.

“Siwezi kusema chochote juu ya hilo, sijui chochote, simfahamu huyo mtu (Iyanya). Kiukweli sijui chochote labda mumpigie yeye mwenyewe kumuuliza”
, alisema Olumide muwakilishi wa Lenovo Nigeria alipozungumza na mwakilishi wa Naija Ghist.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents