Burudani

Iyanya amponda Jaguar amuita ‘mshari na mjivuni’, amsifia Diamond na Sauti Sol

Muimbaji wa Nigeria, Iyanya ameamua kujibu tuhuma alizotupiwa na msanii wa Kenya, Jaguar kuwa hakumpa ushirikiano kwenye video ya remix aliyomshirikisha ya wimbo wake ‘One Centimenter’

Iyanya Jangua

Jaguar alidai kuwa baada ya kushoot video hiyo kwa kubembelezana alimtumia Iyanya ili aisambaze kwenye vituo vya TV nchini humo na kwamba hakufanya hivyo.

Akiongea na Radio Maisha ya nchini Kenya, Iyanya amedai kuwa kutopigwa kwa video ya wimbo huo au wimbo kuchezwa kwenye vituo vya redio kumesababishwa na uzembe wake mwenyewe.

Aliwatolea mfano Sauti Sol na Diamond waliomshirikisha kwenye nyimbo zao kuwa iliwabidi wafanye media tour nchini Nigeria kujitangaza na hivyo kuzifanya nyimbo zao zifanye vizuri kitu ambacho Jaguar alikataa kufanya.

“Diamond alipokuja (Nigeria) tulimpa mtu kutoka kwenye timu yetu aliyemzungusha na kumtambulisha kwenye redio na TV na wimbo wake ukawa miongoni mwa nyimbo kubwa nchini Nigeria kwasababu alikuwa akizunguka kutoka sehemu moja hadi nyingine kujitangaza mwenyewe,” alisema Iyanya.

Iyanya amedai kuwa baada ya Jaguar kwenda Nigeria na wakashoot video alimshauri kufanya hivyo pia ili kujitambulisha na pindi anamwongelea asionekane ‘hayawani’.

“Sijui kama Jaguar alikuwa anategemea mimi nikae hapa na kufanya kazi yake,” aliongeza.

“Kwanini Diamond hajalalamika kuhusu Iyanya? Sauti Sol hawajalalamika kuhusu Iyanya lakini Jaguar amelalamika? Jaguar ni mshari sana na mjivuni,” alisisitiza Iyanya.

Muimbaji huyo pia alikanusha tuhuma za Jaguar kuwa Nigeria haitaki kuzipa nafasi nyimbo za Kenya au Afrika Mashariki kwa ujumla.

Sikiliza zaidi interview hiyo hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents