BurudaniWema Sepetu

It’s All Love: Wema Sepetu na Penny wafanya shopping pamoja (Picha)

Walikuwa marafiki wa damu, wakaja kuwa maadui.. na sasa ni marafiki tena. Baada ya kupatanishwa kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Junaithar siku kadhaa zilizopita, Wema Sepetu na Penny Mungilwa wameendelea kuuimarisha zaidi urafiki wao.

10808749_334389343415649_911133622_n
Penny na Wema

Penny ameshare picha kwenye Instagram akiwa pamoja na Miss Tanzania huyo wa zamani ambayo Wema pia ameirepost kwenye akaunti yake. Hiyo ni picha ya kwanza ya warembo hao wakiwa pamoja kuwahi kuweka kwenye akaunti zao katika kipindi kirefu.

Wakiongea kwa pamoja na Bongo5 leo wakifanya shopping ya nguo, warembo hao wamedai kuwa wana mipango ya kufanya filamu pamoja na wanatarajia kuingia kambini mwakani.

Picha hiyo imepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wao wanaopenda kuwaona wakiwa pamoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents