Burudani

It’s a baby girl: Zari na Diamond wapata mtoto wa kike

Diamond Platnumz na Zari the Bosslady wamepata mtoto wa kike, Latiffah Naseeb Abdul aka Tiffah Dangote.

11356036_1437791433218130_2114438773_n
Mama Diamond akiwa amembeba mjukuu wake, Latiffah pembeni ya mama mtoto, Zari

Mtoto huyo ameingia duniani saa 10 na dakika 40 Alfajir, Alhamis hii.

Haijaweza kufahamika kwa mara moja ni hospitali gani mtoto huyo amezaliwa kwa kile meneja alichosema ‘usalama wa mama na mtoto’ kwakuwa bado wapo hospitali.

“Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah,” ameandika Diamond kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram.

Awali Diamond alisema kuwa Zari angejifungulia Tanzania.

11349200_714483462010913_2119580209_n
Moja ya kabati ya nguo za Latiffah

Tayari mtoto huyo amefunguliwa account ya Instagram iitwayo princess_tiffah.

“Welcome to the Next Most Famous Daughter in Africa… My dad and Mom decided to call me Latiffah but I wanna be called Latty or Tiffah, #Princesstiffa #Lattyplatnumz,” yanasema maneno kwenye picha ya kwanza kwenye akaunti hiyo.

11242009_1478721399110318_1864035948_n

Tunawapongeza mastaa hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents