Burudani

Ishu ya Joh Makini kubebwa sijaiongea kwa ubaya – Young Killer

Msanii wa muziki wa hip hop Young Killer anadaiwa kumdiss msanii wa Hip Hop Joh Makini kwenye wimbo yake mpya ‘Sina Swaga’ akidai kwamba anabebwa kisanaa.

Rapper huyo amedai kuwa hajasema hivyo kwa ubaya bali yeye amezungumza kile ambacho kimekuwa kikizungumzwa mitaani na baadhi ya watu pamoja na wasanii.

“Mimi sijaiongea kwa ubaya, nimeielezea kwa sababu hata Chidi Benz alishawahi kuizungumzia, lakini Joh kwangu ni msanii ambaye namkubali na kama nikisema nimweke kwenye list, tatu bora yupo,” Young Killer alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

Amedai aliamua kuyawakilisha baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakiongelewa na wasanii wengi ikiwemo Chid Benz ambaye aliongelea kwenye media na kutunga mistari inayoelezea jinsi gani Joh anabebwa kisanaa.

Pia rapper huyo alidai kuwa kuna ushaidi mwingi wa picha kwenye blog tofauti zinazoonesha jinsi Joh anavyotuhumiwa kubebwa kisanaa na kusema hana tatizo na Joh Makini na hata akikutana naye atamsalimia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents