Bongo Movie

Irene Uwoya: Mwanangu huwa ananichanganya anavyoomba simu mara kwa mara aongee na Rais Magufuli (Video)

Mtoto wa Irene Uwoya, Krish (6) amekuwa akimsumbua mama yake mara kwa mara kutaka kuongea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Uwoya amedai kuna wakati anamrekodi video na kumdanganya kwamba anamtumia Rais Magufili ili kumtuliza mtoto huyo.

“Mara nyingi huwa ananiambia mimi nampenda sana Rais Magufuli, natamani kuwa Rais, anaongea hivyo, yaani muda mwingine nakuwaga nachanganyikiwa,” alisema Irene Uwoya. “Anaweza akaniambia Mama una namba ya Mh Rais Magufuli, naomba kuongea naye,”

Alisema kunawataki mtoto huyo anaomba arekodiwe video ili atumiwe Mh. Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents