Bongo Movie

Irene Uwoya kufanya usaili wa dancers watakaotumika kwenye filamu yake mpya

Muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya amesema anaandaa filamu yake mpya yenye dance nyingi ndani yake,ambapo atafanya audition kwa vijana wenye uwezo wa kucheza.

Irene

Akizungumza na Bongo5 leo, Uwoya amesema akishawapata vijana wenye uwezo wa kucheza atawatumia kwenye filamu hiyo Pamoja na kwenye kipindi cha Paradise.

“Kwa movie ambayo naiandaa ni ya dance inachanganya muziki,dance na movie. Kwahiyo nitafanya audition very soon ya vijana wenye uwezo wa kucheza, watakuwepo kwenye movie hiyo na baadaye tutawatumia kwenye Paradise. Kwahiyo vijana wakae mkao wa kula,” amesema.

“Unajua tunahitaji kufanya vitu tofauti kidogo,kwahiyo hii ni filamu ambayo itakuwa na muziki ndani yake,ndio maana nimesema itakuwa na dance ambayo watafundishwa nini cha kufanya katika filamu hiyo ambayo imeanza kuandaliwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents