Burudani

Inspector Haroun kuachia track 3, azungumzia ujio wa album mpya ya ‘Sharubu za Babu’

Mfalme wa Rap Katuni, Haroun Kahena ‘Inspector’ amesema anatajia kuachia track tatu kabla ya ya kuachia album yake mpya ya ‘Sharubu za Babu’.

Inspector-Haroun-By-Mitaaflani

Inspector amesema ana kazi nyingi alizofanya na wasanii mbalimbali wakiwemo Domokaya na Juma Nature ambazo zitatoka na nyingine zitakuwa kwenye album hiyo.

“Domokaya alinitafuta akaniambia iko haja ya kufanya kolabo ,so akanipa idea nikamwambia sina tatizo kwa sababu muziki wetu unafanana nikamwambia tunawezafanya,” ameiambia Bongo5. “Kwahiyo tukamtafuta producer mmoja anaitwa Duppy tukafanya mkono wa kwanza, lakini yeye anahitaji tufanye ngoma nyingi nyingi, kwahiyo ni project endelevu tutakuwa tunafanya kama kolabo ambazo yeye ataweza kuzitumia na mimi nitaweza kuzitumia, kama ilivyokuwa ‘Hakuna Noma’ ya Professor, Ispector na wengine walikuwa wanaitumia,” ameongeza.

“Hii ni kolabo ambayo ina manufaa kwa wote pia hizi ngoma zitakuwa kwenye albUm yangu mPya ‘Sharubu za Babu’ pamoja na ngoma nyingine ambazo nimefanya na Juma Nature. Pia kuna ngoma inaitwa ‘Kaleligo Ukae’ inamaana kuna mtoto wa kike kalelewa vizuri ‘binti wa kizaramo’ mimi mama yangu ni mzaramo nimejaribu kukumbuka lugha ya nyumbani kidogo kwa upande wa mama yangu, hiyo ni ngoma yangu itatoka, nataka ku release ngoma tatu hewani kwa sababu maswali yamekuwa mengi mtaani baada ya Sharubu za Babu watu wameniona kimya sana. Lakini sio ukimya labla sina ngoma, nina ngoma na zitaanza kutoka baada ya Ramadhan. Kwahiyo ngoma zitatoka na album pia itatoka baadaye.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents