Burudani

Illuminati? Godzilla aeleza undani wa single yake mpya ‘Illuminaughty’

Wiki Godzilla anaachia ngoma kadhaa ukiwemo wimbo rasmi uitwao ‘Karibu Yako’ uliotayarishwa na Lamar pamoja na wimbo usio rasmi uitwao ‘Illuminaughty’.

IMG_71181

Godzilla amedai kuwa pamoja na Illuminaughty kufanana na Illuminati ambayo huhusishwa na shetani, watu wasiogope kwakuwa anachohitaji ni kufikisha ujumbe wake kwa jamii.

“Unajua kuna wazazi ukiwapelekea mke unakuta yale mavazi ya vimini, kujipodoa, watakwambia ‘mbona umetuletea shetani nyumbani’, lakini unakuta mapenzi hayaangilii mtu yukoje, wala jinsi alivyo,” amesema Zilla. “Kwahiyo wao wazazi wanamwita shetani lakini sio shetani, sema wimbo sio Illuminati, Illuminati inawakilisha shetani, lakini naughty sio shetani. Kwahiyo mzazi anaweza akamuona demu wako akasema huyu ni shetani kabisa, ukamjibu ‘huyu sio ni mwonekano tu’, huyu sio shetani, huyu ni mtu mzuri na ana moyo mzuri,” ameongeza rapper huyo.

Hata hivyo Zilla amesema video yake lazima iwe ya kishetani.

“Video yake lazima iwe ya kishetani kweli, kutakuwa na design za devil sign zote yaani, lakini huyu mtu ni mtu mzuri. Kwahiyo kutakuwa na watu wenye mapembe, yaani ukiiona unaweza jua huyu ni shetani. audio itatoka kesho lakini video itatoka soon na nitashoot na Nick Dizzo.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents