Burudani

‘Iggy Azalea aliumizwa na maneno ya Nicki Minaj kwenye tuzo za BET’ asema boyfriend wake

Pamoja na rapper mwenye asili ya Australia, Iggy Azalea kudai kuwa hakusumbuliwa na maneno ya Nicki Minaj kwenye tuzo za BET mwishoni mwa mwezi uliopita, mpenzi wake Nick Young anayecheza kikapu na timu ya Los Angeles Lakers, ameliambia New York Daily News kuwa kauli ya Nicki na maneno ya watu mtandaoni, vilimuumiza ‘demu’ wake huyo.

Model-Athlete-Nick-Young-and-Iggy-Azalea-In-Versace-Versace-Versace-for-GQ

“Iggy anafanya vitu vikubwa na hicho ndicho kinawaogopesha watu. Atayapuuzia tu. Hawezi kukubali yamharibie. Yupo namba moja, utafanya nini? Yupo juu sasa hivi, hivyo lazima watakufuata,” alisema. “Ilinibidi nishughulike na matokeo yake aliporudi nyumbani na alikuwa akipitia simu yake, akisikia kila mtu akiongea mbovu kumhusu. Nilihakikisha nipo pale kwaajili yake,” aliongeza.

nicki-minaj-bet-awards

Hata hivyo Nicki Minaj alidai kuwa kauli yake wakati anapokea tuzo za ya rapper bora wa kike kuwa yeye huandika mashairi yake mwenyewe haikumlenga Iggy na kwamba vyombo vya habari ‘vilimwekea maneno mdomoni’.
Kupitia Twitter, Nicki aliandika:

“I’ve congratulated Iggy on the success of ‘Fancy,’ publicly. She should be very proud of that. All women nominated should be proud. That will never change my desire to motivate women to write. Our voices have to be heard. I hope I inspire up & coming females to do that.”

Naye Azalea, alitumia Instagram kusema alivyoyachukulia maneno ya Nicki na kudai kuwa hayakumsumbua:

“Generally speaking I’m unbothered by anything that “happened” at the BET awards and just feel worn out by everyone trying to make me have wars with people all the time…I hate to see everyone exhausting themselves on my behalf over things I’m still not 100% sure even exist & don’t matter. just let it go.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents