Burudani

Iggy Azalea akanusha kuwahi kuolewa! Ex wake adai kumpa talaka

Rapper Iggy Azalea amekanusha kuwahi kuolewa miaka ya nyuma na mpenzi wake Hefe Wine.

rs_634x813-140421161240-634.igg7.cm.421143

Mtandao wa TMZ uliripoti kuwa mpenzi wake wa zamani, Wine (aka Maurice Williams) alidai kuwa alifunga ndoa na Iggy kwa sheria za kijamii ‘common law marriage’ na amempa talaka. Kwenye maelezo yake Wine anasema Iggy alikubali kuolewa na wakaishi kama mume na mke huko Texas September, 2008. Anadai kuwa walianza kuishi mbalimbali mwaka jana.

Kwenye jimbo la Texas, mwanaume na mwanamke wanaoishi pamoja kwa muda mrefu wanatambulika kuoana kisheria. Hefe anamtaka jaji kumkataza Iggy kuuza mali walizokusanya wakati wa ‘ndoa’ yao. Kama jaji akiitambua ndoa hiyo, muziki wote aliorekodi Iggy katika kipindi hicho utagawanisishwa 50/50.

Iggy amekanusha taarifa hiyo kupitia Twitter:

“I think we already all know, but just to clarify. I’m NOT married. Feel free to check the PUBLIC marriage records. Gotta laugh tho, now do you see the kinda craziness I deal with?! #ThisLifeWeLive.”

“TMZ just asked me at the airport if I think my “common law marriage” claim is a money grab. Yes, but it’s TMZs money his grabbing. Lol. Press don’t care that a story is clearly false, they just want you to click it. So they’re happy to pay, and this person continues to make $.”

Iggy ana uhusiano na mchezaji wa Lakers, Nick Young. Awali Hefe alitishia kusambaza mkanda wa ngono waliorekodi pamoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents