Ifahamu TV1: Kituo kipya cha TV, Tanzania kinachomilikiwa na kampuni ya Sweden (MTG) kitakacholeta mapinduzi ya vipindi vya burudani
ITV, EATV, Channel Ten, Star TV na vituo vingine vya runinga Tanzania vimepata mpinzani mwenye nguvu. Ni kituo kipya kiitwacho TV1. Kituo hicho kinamilikiwa na kampuni ya Sweden iitwayo, Modern Times Group.
Logo ya TV1
Kampuni hiyo iliyojikita zaidi kwenye masuala ya burudani imeanzisha kituo hicho mapema mwaka huu na kwake ikiwa ni TV ya kwanza ya bure kuwahi kuianzisha.
Newsroom ya TV1 iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam. Channel hiyo tayari inaonekana kupitia ving’amuzi vya Startimes na inawafikia asilimia 38 ya wananchi wa Tanzania
George Tyson, director wa vipindi wa TV1
TV1 itakuwa ni channel ya burudani itakayokuwa pia mchanganyiko wa habari zilizoandaliwa nyumbani na za kimataifa pamoja kurusha filamu za kimataifa na TV series.
Vanessa Mdee akiwa kwenye set ya show yake ‘The One Show’ ya kituo hicho
Vanessa Mdee akifanyiwa make-up
Vanessa Mdee
TV1 ni channel ya pili ya bure ya kampuni ya MTG iliyoanzisha barani Afrika, baada ya kituo cha Viasat1 kilichopo nchini Ghana kilichoanzishwa mwaka 2008.
Watangazaji wa habari wa TV1, Nzowa na Agnes
Tayari kituo hicho kimeajiri watangazaji mbalimbali wazoefu kufanya vipindi mbalimbali wakiwemo Marygoreth Richard aliyekuwa msomaji wa habari za East Africa Radio, Angel Karashani (TPF6) na aliyewahi kuwa mtangazaji wa Channel Ten, Nzowa
Angel Karashani