Burudani

Idris Sultan asema amekoma kuweka wazi mkwanja anaoingiza kwenye deal anazosaini

Mchekeshaji Idris Sultan amefunguka kwa kusema kuwa sasa hivi hatoweka wazi tena kiasi cha pesa ambacho atakuwa anaingiza kwenye deal mbalimbali anazosaini.

Mshindi huyo wa BBA 2014 ambaye hivi karibuni alisaini deal ya balozi wa amani Tanzania, amedai baada ya wananchi kujua pesa ambazo aliingiza kupitia BBA kulisababisha mambo mengi kutokea.

“Kusema kweli siwezi kuweka wazi hela ambazo naingiza kwenye deal ya ubalozi lakini ni pesa nzuri sana, ningependa watu wanifuatilie mimi, hizi ishu nyingine waachane nazo kwa sababu ile ishu ya BBA ilizungumziwa sana. Yaani baada ya watu kujua napewa kiasi gani ilikuwa tatizo sana,” alisema Idris.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents