Burudani

Idris aeleza kwanini yeye na Wema hawakurupuki kufunga ndoa

Idris Sultan amesema ni mapema sana kufunga ndoa na mpenzi wake Wema Sepetu ambaye kwa sasa ni mjamzito.
Wema na Idris

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Idris amesema bado mahusiano yao yanaitaji muda zaidi ili kujiandaa vizuri kuingia kwenye ndoa.

“Ndoa nilisema inshallah lakini bado haipo kwenye mpango,” alisema Idris.

“Unajua ni vizuri ukiwa kwenye mahusiano na mtu, usiweze kukurupuka kufunga ndoa, ndio maana unakuta kuna ndoa nyingi zinavunjika. Inabidi mjuane, muelewane na muone kabisa kwamba kuna haya kadhaa ambayo nitakubaliana nayo au haya sitakubaliana nayo, so mnakubaliana kwanza. Kwahiyo mkishakubaliana kabisa kuingia kwenye ndoa mnakuwa tayari na mnajuana kabisa,” aliongeza Idris.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents