Burudani

Ice Cube awa-diss MTV kwa kumpa tuzo Paul Walker badala ya kupewa yeye

Rapper wa siku nyingi ambaye pia ni muigizaji Ice Cube ameonesha kutoridhishwa na ushindi aliopewa muigizaji wa Fast & Furious marehemu Paul Walker, katika tuzo za ‘MTV Movie Award’ katika kipengele walichopangwa pamoja cha ‘Best Onscreen Duo’.

ICE CUBE

Paul Walker na Vin Diesel ndio walitajwa washindi wa kipengele hicho katika tuzo hizo zilizotolewa April 13 kitu ambacho Ice Cube hakukifurahia.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na USA Today, Ice Cube alisema:
“We had the best chemistry of everybody nominated, for us not to win was crazy, They should have gave it to him before he passed away.”

Hata hivyo baada ya habari hiyo kuandikwa na mitandao mbalimbali na mashabiki wa Paul Walker kumshambulia, Ice Cube alizungumza kupitia twitter:

“I would never diss the actors who won. Not even Paul Walker. Seriously people! [Regarding] The sympathy vote: We should honor people before they die. That’s all. Shame on you […] reporters.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents