Technology

Huu ni mwisho wa Ipod? Mauzo ya kifaa hicho cha kusikilizia muziki yashuka kwa zaidi ya nusu

Kifaa maarufu cha kusikilizia muziki cha kampuni Apple, Ipod, ambacho kilisababisha kifo cha kifaa cha kampuni ya Sony, Walkman – nacho kinakabiliwa na kifo chake chenyewe.

IPod_family

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya hivi karibuni, Apple iliuza iPod milioni 6 kwenye robo ya kwanza ya mwaka jana na kuonesha kuwa mauzo yameshuka kwa asilimia 52 ukilinganisha na mwaka uliopita. Kwa sasa mauzo ya iPod yanaingiza asilimia 2 tu ya mapato ya kampuni ya Apple.

Kushuka kwa mauzo ya vifaa hivyo yanadaiwa kutokana na kuongezeka kwa apps za muziki kwenye simu, mitandao ya kuhifadhia muziki mtandaoni na kuchezea muziki kama Spotify. Kingine simu za iPhones huja na iTunes na kufanya iPod zikose kazi kwa watumiaji wengi wa iPhone.

Mauzo ya iPod yalikuwa makubwa zaidi mwaka 2008 kufuatia kuanzishwa kwa iPod Touch mwishoni mwa mwaka 2007. iPod Touch iliyotengenezwa kuonekana kama iPhone, ilikuwa ikicheza muziki na kuwa na apps, lakini haikuweza kupiga simu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents