Burudani

Huu ndio muda wetu wa kurudisha heshima – Yamoto Band

Yamoto Band wiki hii wanajipanga kuachia wimbo wao mpya baada ya kumaliza tour yao ya kimataifa ambayo waliifanya katika mataifa 6.

Bendi hiyo ambayo imekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia project mpya, wiki hii itaachia kazi mpya kwa mujibu wa mkurugenzi wa bendi hiyo, Mkubwa Fella.

“Mashaki watulie tu, muda wetu umewadia kabisa, ndani ya wiki kitu kipya tunaachia,” alisema Fella.

Alisema maandalizi ya project za bendi yako tayari na kwa sasa wanasubiri muda muafaka wa kuziachia tu.

Waimbaji hao bado kwa sasa wanafanya vizuri na wimbo wao Su.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents