Burudani

Huu ndio mkwanja uliotumika kushoot video ya ‘Kaunyaka’ ya Chege na Temba

Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fella amesema waliamua kumtumia Adam Juma kushoot video za Kaunyaka ya Chege na Vuvula ya Madee kwakuwa ni mtu wanayeamini ubora wa kazi yake.

10919100_282718041852156_79790684_n

Video hizo zilifanyika nchini Afrika Kusini.

“Kwanza video ya Kaunyaka imegharimu shilingi milioni 11,” amesema Fella.

“Tumemchukua Adam Juma mpaka kule lakini ametumia vifaa vya wa Afrika Kusini na toka nimjue Adam ni mtu ambaye ni mbunifu na anaweza na ndio maana tuliamua kumchukua ili akawaelekeze wazungu na tukaamini watafanya kitu kizuri sana ndio maana tumemchukua mtanzania mwenzetu kwa sababu anajua changamoto ya muziki wetu,” Fella alikiambia
kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Mbeya.

Video hizo zitazinduliwa Kwa February 7, Escape One.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents