Burudani

Hutaamini alichojibu Harmorapa kuhusu jinsia yake!

Rapa Harmorapa anaendelea kutawala mitandao ya kijamii kila kukicha kutokana na vituko vyake. Jumatano hii amewaacha mdomo wazi baadhi ya mashabiki wake baada ya kutoa jibu tofauti kuhusu jinsia yake.

Akichat na mashabiki katika mtandao wa facebook wa EATV ndani ya segment ya Kikaangoni, rapa huyo aliulizwa swali kuhusu jinsi yake ‘Wewe ni mwanaume wa aina gani?’ na rapa huyo kujibu ‘Mimi ni strong woman’.

Jibu hilo limewashangaza mashabiki wengi wa rapa huyo kwa kuwa wanajua yeye ni mwanaume huku wengine wakidhani huwenda hakuelewa swali kutokana na lugha ya kingereza iliyotumiwa.

Akiongea kuhusu uwezo wake wa kuongea na kuandika lugha ya kingereza alisema: “Lugha ya Kiingereza naifahamu vizuri lakini ile kuongea ongea ndiyo siwezi”

Rapa huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Kiboko ya Mabishoo’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents