BurudaniDiamond Platnumz

Hussein Machozi asema wimbo wa ‘Mdogo Mdogo’ uliovuja aliurekodi miaka 2 iliyopita kabla Diamond hajatoa wake, adai hana beef nae

Wiki iliyopita kuna wimbo mpya wa Hussein Machozi wenye jina la ‘Mdogo Mdogo’ ulisambaa kwenye mitandao, huku mtandao wa GHAFLA wa Kenya ukiupambanisha na ‘Mdogo Mdogo’ ya Diamond na kuamsha hisia kuwa huenda ni beef inayoanza kutokota jikoni.

huss2

Hussein Machozi ameiambia BONGO 5 kuwa wimbo huo alikuwa hajapanga kuutoa kipindi hiki bali umevuja.

“Yeah kuna wimbo upo masikioni mwa watu sasa hivi ambao haukupangwa kutoka hivi karibuni ila nashangaa kuukuta mitandaoni yaani umevuja”.

Hit maker huyo wa ‘Kwa Ajili Yako’ amesema kuwa wimbo huo ameurekodi miaka miwili iliyopita, na si kama ambavyo watu wanadhani kuwa huenda ameutoa kumjibu Diamond.

“Wimbo umerekodiwa miaka miwili nyuma na sikuwa najua kama Diamond nae ana wimbo kama huo. Wakati naufikiria kuutoa ndio nikasikia Diamond ametoa wakwake nae ameuita mdogo mdogo. Nilijaribu sana kubadilisha jina ila haikuwezekana kulingana na maana nzima ya wimbo, mimi nikauacha nikasema wacha niutulize hadi ya bwana Diamond ipite nami nitautoa wangu, ila nimeukuta kwenye mitandao sina jinsi.”

Kuhusu nani anayehusika kuuvujisha na hatua zozote alizochukua:

“Nadhani ni producer maana hakuna aliyewahi kua nao huu wimbo zaidi ya mimi na producer Toti. Sijachukua hatua zozote zaidi ya kumuuliza na alivyokataa basi nikawa sina jinsi tena maana tayari watu wanao sasa huu wimbo siwezi waambia rudisheni au uacheni, nimeuacha uende tu.”

Kuhusu sababu anazohizi zimefanya wimbo wake upambanishwe na mdogo mdogo ya Diamond, je ni kweli ana beef nae?:

“Hapana mimi sinaga beef na mtu kwa kweli beef labda kikazi tu, mimi naona sio mbaya maana sisi ni wanamuziki na hiyo ni kazi yetu na wao pia wamefanya kazi yao ambayo wanaona inawafaidisha wao, angekuwa mtu mwingine au wimbo ni wa kawaida tu wasingeweza kumuweka hapo na Diamond au kumuandika kivyovyote. So wameona mimi nastahili na pia inastahili ni kali namaanisha ndio maana wameiweka hapo, mimi naona ni sawa tu”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents