Burudani

Hupendi Kiingereza? Hizi ni sababu za kwanini unajitengenezea wakati mgumu

Lugha ni nyenzo ya mawasiliano kwa watu mbalimbali katika jamii tofauti tofauti. Mawasiliano hayo ndio yanayofanya mambo yaweze kufanyika katika mila na desturi mbalimbali, hivyo basi hakuna namna tunaweza kuepuka lugha yeyote katika jamii zinazotuzunguka.

work1

Kitu cha msingi unachotakiwa kujua je lugha hii ina umuhimu kiasi gani na inaathiri vipi maisha yangu binafsi? Tupo watanzania wengi tusiopenda kuona watu au vijana wanaongea Kiingereza kwa kisingizio kwamba wanapuuza lugha ya kiswahili na maneno mengi yanayoambatana na hayo.

Hawajakosea na hakuna mtu anatakiwa kupuuza lugha yake kwa msingi wa kwamba akashindwa kuwasiliana na watu wengine kisa anapuuza lugha yake. Na mtu wa namna hiyo bado sijakutana naye isipokuwa wale ambao wanaongea kiswanglish!

Unatakiwa ujue faida ya kujua lugha zaidi ya moja Tuna vijana wengi ambao ni wajanja wa mjini lakini Kiingereza kina wapiga chenga kwasababu hawajaamua kuchukua hatua ya kujifunza au wakiwa shule waliamua kumkimbia mwalimu wa Kiingereza ingawa mwalimu hakuwa mzuri sana bali wangekaa wangetoka na chochote. Mwenda bure si mkaa bure, namaanisha kwamba unapojua lugha zaidi ya moja kama Kiingereza, kifaransa, kiaarabu, kichina n.k unajiweka kwenye upeo wa kupata fursa nyingi zaidi kuliko mtu anayejua kiswahili peke yake.

Malengo yako unataka kufika nayo wapi? Kama una malengo ya kufika vijijini maisha yako yote, basi lugha kuu itakuwa kiswahili na lugha za kabila za watu unaowatembelea kila mara. Sijawahi kuona mtu anasemwa vibaya kwa kujifunza kinyakyusa wakati yeye si wa kabila hilo. Kama unajua lugha yako unaijua tu hakuna mtu atakayeichukua kutoka kwako. Kujua lugha nyingine inakuongezea ufahamu wa kujua tamaduni na maisha ya watu mablimbali duniani.

Kama wewe ni mfanyabiashara huwezi kukwepa kiingereza Mfanyabiashara anayekwepa kujua kiingereza na lugha zingine za kimataifa ni sawa na kujifungia jela yako mwenyewe wakati wengine wako huru. Tunatarajia biashara yako kukua na kuongezeka hivyo si kila mteja wako ataongea kiswhili hivyo unatakiwa kujiandaa kwa kila hali. Usiogope kusemwa kwamba umepuuza lugha yako, hao wanaosema unang’ang’ania lugha za wageni wao wanazijua vizuri na hata watoto wao wanasoma English media.

Naomba tukubaliane kutokubaliana kwamba hutoweza kukwepa au kupambana na kiingereza inabidi ujiunge na ujifunze na taratibu vita yako itaisha. Vijana wetu wengi wanashindwa kusimama hasa kama kuna usahili unaohusisha lugha ya kiingereza na hakuna anayewasaidia kuweka juhudi kujifunza.

Ushauri wa bure, kama lugha ya kiingereza inakupiga chenga anza kujifunza sasa maana tunakokwenda hutoweza kushindana kwa ujasiri hasa unapokutana na wengine ambao si watanzania. Tunahitaji kujijengea ushindani binafsi na kuacha kulalamika kuhusu shule uliyosoma au mfumo uliotumika. Huwezi kubadilisha kilichotokea nyuma yako bali unaweza kubadilisha kitakachotokea mbele yako.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents