Tragedy

Huku Waghana wakiomboleza, Dramani Mahama aapishwa kama rais mpya wa Ghana



Makamu wa rais wa Ghana John Dramani Mahama ameapishwa kuwa rais mpya wa Ghana kufuatia kifo cha rais John Atta Mills.
Dramani aliapishwa kama rais mpya wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwenye sherehe iliyorushwa live kwenye vituo vyote vya runinga nchini humo.
Muda mfupi baada ya Dramini kuchukua madaraka aliagiza bendera kupeperushwa nusu mlingoti kwa kipindi cha wiki nzima kama maombolezo ya kifo cha rais Atta Mills.
Mpaka sasa sababu za kifo cha rais huyo haijafahamika mapema.
Kifo chake kimekuja siku chache tu baada ya kutangaza nia ya kugombea tena urais mwezi December mwaka huu.
Rais Atta Mills amefariki akiwa na miaka 68.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents