Burudani

Huenda Rwanda ikashiriki kwenye Big Brother Africa Hotshots

Kuna habari za uhakika kutoka kwenye vyombo vya habari vya nchini Rwanda kuwa huenda nchi hiyo ikashiriki kwenye shindano la Big Brother Africa.

bba

Kwa mujibu wa gazeti la The New Times la Rwanda washiriki kutoka huko wanaweza kuingia kwenye jumba la shindano hilo ikiwa ni wiki tatu baada ya kutangazwa kuwa imeondolewa kutokana na masuala ya visa.

Ingawa M-Net AfricaMagic haijatoa tamko rasmi, Waziri wa utamaduni na Michezo wa nchi hiyo, Joseph Habineza amethibitisha kuwa suala la visa limefanyiwa kazi na washiriki wa Rwanda wanaweza kwenda Afrika Kusini.

“Tumepokea habari za ushiriki wa Rwanda kwenye show ya Big Brother. Ingawa BBA ni shindano binafsi, tuna uhakika kuwa wawakilishi wetu watatumia show hiyo kutangaza utajiri wa Rwanda,” alisema Habineza.

Big Brother Africa inatarajiwa kuanza October 5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents