Habari

Hospitali MOI kushtakiwa kwa upasuaji mwenye utata

NDUGU wa Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji tata katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wako katika hatua za mwisho kuishtaki serikali mahakamani.

Na Jackson Odoyo

 

NDUGU wa Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji tata katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wako katika hatua za mwisho kuishtaki serikali mahakamani.

 

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya serikali kusema kwamba endapo ndugu wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji tata Novemba mosi mwaka jana MOI hawataridhika na huduma walizopewa wafuate mkondo wa sheria.

 

Wagonjwa hao ni Emmanuel Didas (19) aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu na Emmanuel Mgaya (20) ambaye kwa sasa ni marehemu aliyepasuliwa mguu badala ya kichwa.

 

Akizungumza kwa simu jana jijini Dar es Salaam, mjomba wa marehemu Emmanuel Mgaya, Dismas Mgina alisema kabla ya yote serikali inapaswa kutambua kwamba kulipa fidia ni wajibu wao kabla ya wao kufungua kesi mahakamani kutokana na uzembe uliofanywa na madaktari.

 

Mgina ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Anglikana, mkoani Iringa alisema mbali na hilo suala la kushtaki ni haki yao kwani wanaruhusiwa kisheria kufanya hivyo na kwamba walikuwa na wazo hilo kabla ya serikali kutoa kauli yake.

 

Mjomba mwingine wa marehemu Mgaya aliyezungumza na Mwandishi wa habari hizi ni Dk Clarence Mgina na kusema kwamba hata wao waliitegemea kauli hiyo ya serikali na walishanza maandalizi ya kufungua kesi na kwamba sasa wako katika hatua za mwisho kwani wameshampata wakili (mwanasheria) wa kusimamia shauri hilo.

 

Naye msemaji wa familia ya mgonjwa Emmanuel Didas ambaye pia ni kaka yake, Sistis Marishay alisema walikuwa wanasubiri kauli ya serikali ndipo wachukue hatua zinazostahili.

 

Wanafamilia tunategemea kukutana wakati wowote kuanzia sasa kujadili suala hilo, alisema Marishay.

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents