Habari

Hoja za Zitto baada ya Rais Magufuli kusema nchi haina njaa

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ametoa hoja zake baada ya Rais Dkt John Mafuguli kusema kuwa nchi hii haina balaa la njaa.

Zitto ameyaainisha hayo katika ukurasa wake wa Facebook kama ifuatavyo:

Rais umeamua kuchagua upande wa wanaokupa Taarifa za uwongo na majungu. Muda utasema. Wengine tumesema, tumeonya kwa mapenzi mema ya nchi. Wewe ndio mwenye vyanzo vingi na mkono mrefu. Umetamka hakuna njaa. Umefunga mjadala. Lakini uwe tayari kubeba mzigo wa maamuzi yako yanayotokana na habari za majungu, uwongo na kutaka kukufurahisha.
Anayejua kuna njaa nchi hii ni Rais,mimi ndio naejua wapi kuna njaa na wapi hakuna.Tanzania hii haina njaa wala watu hawana njaa,anasema Rais JPM kutoka Simiyu
Wanaotangaza kuna njaa ni watu wanaolipwa pesa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kusema nchi ina njaa na ukame wa kuuwa watu na mifugo.
=========
Yapo magazeti yanayotumiwa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kusema Tanzania kuna njaa.Kuna mfanyabiashara mmoja ana tani elfu25 za mahindi bandarini anataka aingize bila kodi kwa kisingizio cha njaa Tanzania,Rais anasema ameagiza alipe kodi na asipitishe mahindi hayo bure kwa kisingizio cha njaa,Tanzania haina njaa.

Kuna mfugaji mwingine walimlipa hela wanasiasa huko Mvomelo,akaenda mbele ya Tv na kusema ana mifugo inakufa kwa ukame.Nimeagiza wamwambie auze hizo ng’ombe ili aepukane na ukame.Huwezi kuwa na ng’ombe karibu elfu na zaidi na wanakufa ng’ombe 16 unaanza kulialia badala ya kuuza upate hela ya kula na ujikimu kimaisha.

Rais anasema hatapeleka chakula Simiyu na Bariadi eti kisa ukame.Wananchi walitakiwa kujua kama mvua ni ndogo basi walime mazao yanayostahimili ukame na si kulazimisha kulima mahindi yanayohitaji mvua nyingi.JPM anasema msema ukweli ni mpenzi wa Mungu,na yeye anasema ukweli kuwa hataleta chakula popote kwa sababu ni wanasiasa na wafanyabiashara ndio wananunua magazeti kutangaza njaa.
Rais kamuumbua Dr Kamani,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu anayemtaka Rais aruhusu kuingiza mifugo kwenye hifadhi,wakati yeye akiwa waziri wa Mifugo wakati wa JK hakufanya hivyo,sasa kama sio unafiki ni nini?JPM anasema yeye sio mnafiki,hataruhusu mifugo kuingia kwenye hifadhi kwa sbb ya sifa za kisiasa huku akiharibu mazingira.

Rais anasema Watanzania walizoea kuambiwa maneno “matamu matamu” na wanasiasa huku muda ukienda bila kuwa na maendeleo.Yeye anataka watanzania wasahau maneno matamumatamu.Ataongea ukweli tu,tena ukweli mchungu hata kama utawaudhi watu,kama ni jiwe atasema jiwe na sio mchanga mgumu uliokusanyika pamoja.

Rais amewaomba Watanzania wazidi kumuombea,wapo “wapinzani” wake wanamsimanga kwa kununua ndege,na wakati kwa miaka mingi Tanzania haikuwa na ndege,na hao wanaomkosoa ndio hao hao wanaokimbilia kuzipanda.

Baadae Rais akamuita mhandisi Maji wa Mkoa wa Simiyu ili aje aelezee mpango wa Maji kutoka Ziwa Victoria kuja mkoa wa Simiyu na Wilaya zake…Mhandisi hakutoa majibu mazuri,akaja RAS ambaye akasema kikwazo ni mlima wa Ngasamo ambao una madini ya Nikel(?)ambao ndio ilipaswa kuwa na tank la kuleta maji.Eneo hilo tayari kuna muwekezaji na hawawezi kuweka tank.

Rais ameamuru mgodi huo usipewe leseni na huyo muwekezaji apewe taarifa kuwa huo mgodi haupo tena na watu wapewe eneo la kuweka Tank.Amemuagiza Kamishna wa madini aifute leseni na ujumbe umfikie Waziri wa Madini na autekeleze.

Na mwisho Rais amesisitiza watu wafanye kazi,hakuna wa kugawiwa chakula bure.Hawezi akawasomeshea watoto bure,ajenge barabara,anunue ndege,ajenga hospital na kuweka madawa ktk hospital,alete huduma ya maji na bado watu wakae tu na kusubiri eti serikali itawatafutia chakula.Watu wafanye kazi ili wapate chakula na si kusubiri chakula cha serikali.”SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA,NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI KWELI,WALA SIMUNG’UNYI MANENO NA SITALETA KWELI,MLIZOEA MANENO MATAMU SASA MIMI SINA MANENO MATAMU”alisisitiza Rais Magufuli.

Mwishoni Rais amemalizia kwa kusema “Naweza kuwa sio mwanasiasa mzuri sana,Lakini ipo siku mtakuja kunikumbuka”

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents