Habari

Hizi ni tabia tano za dereva mzuri wa basi

Kila abiria ana habari tofauti kuhusu dereva na safari aliyokutana nayo. Ukiondoa madereva wasiojali na wenye kusababisha ajali nyingi kwenye barabara zetu za bongo. Hebu tuangalie dereva mzuri na tabia au hulka yake inatakiwa iweje;

Bus+driver+Galpotthawela

Kila dereva anatakiwa kujali na sio kuendesha tu gari.Kuwa dereva ni kwenda zaidi ya majukumu yako ya kazi kuhakikisha kila abiria anapata na kuwa katika hali nzuri ndani ya gari hiyo. Kuna tabia nyingi ambazo zinakufanya uwe dereva mzuri? Kama unataka watu wakufurahie, wakuthamini, na wewe uwe na ujasiri kwenye kazi yako unahitaji vitu hivi hapa;

  1. Uwe Mtu Mwenye Utu

Kama dereva unawakilisha mwenye gari au kampuni inayomiliki basi hilo. Wakati unapoendesha basi hilo kila kitu unachokifanya na namna unavyoongea na abiria unawakilisha kampuni hiyo. Kama utawahudumia na kuongea na watu vibaya na kufanya vitu vya ajabu ndivyo watu watakavyo litizama kampuni hilo au basi hilo.

  1. Unatakiwa kuongoza

“Dereva ni kiongozi hivyo wakati wote wanaongoza safari na watu wafanye nini au wasafirije. Kitu ambacho unatakiwa kujua umepewa mamlaka ya kuongoza abiria hao kwa masaa kadhaa, hivyo chukua nafasi yako na ujasiri wa kuwaongoza kuhakikisha wanafika salama. Kama kuna utaratibu kuhusu basi lenu, dereva ndio mtu muhimu wa kutoa mwongozo, kusimamia usalama na kuhakikisha abiria wanaridhika na huduma ya basi hilo,” anasema mtu mmoja.

  1. Kuwa Mtulivu na mwenye Mwelekeo Wakati wa Shida

Madereva wa mabasi hawana nguvu ya kuwamiliki watu waliowazunguka wakati wa safari. Hivyo wanatakiwa kuwa tayari kufanya chochote mtu akiingilia anga zao.

Changamoto ambazo wanakutana nazo ni kama;

  • Hali mbaya ya hewa
  • Abiria wasumbufu
  • Usumbufu wa Askari wa Barabarani
  • Barabara mbaya wakati mwingine, inategemeana na Safari unakwenda wapi

Kama dereva wa basi jambo la msingi ni usalama wa abiria na kuhakikisha unawafikisha salama. Hivyo kuwa makini na mtulivu wakati wa shida au jambo Fulani linapotokea ni muhimu sana kwa dereva mzuri.

  1. Wamejitolea kufanya kazi Hiyo ngumu.

Unapokua unajitambua na unapenda kazi hiyo inaongeza furaha katika kazi yako. Watu wengi tunatumia masaa nane ya maisha yetu katika kazi hivyo unahitaji kupenda unachofanya. Kwa dereva yeyote utulivu na kujiamini anapokuwa kwenye usukani ni muhimu, hutakiwi kuwa mtu mwenye mawazo au unayeongoza na hisia nyingi. Unatakiwa ni mtu mwenye kuzingatia kila jambo unapokuwa barabarani, na ujue wewe ndio sababu ya kampuni hiyo kupendwa au kuchukiwa.

  1. Anahitaji kuwaheshimu watu wengine

Kama ilivyo kwa kiongozi mzuri wakati wa kutengeneza timu nzuri unahitaji kuwaheshimu watu unaofanya nao kazi. Hivyo hivyo kama dereva lazima kuwaheshimu watu unaofanya nao kazi kama wasaidizi wako, kwani endapo kitu kikatokea mkiwa barabarani hautaweza kurekebisha peke yako , unahitaji watue wengine.

Heshima hiyo inawatengenezea abiria uwezo wa kusafiri na wewe wakati mwingine.

Je wewe ni dereva?

Hiyo ni taaluma kama taaluma nyingine ambayo unaweza kubadilisha maisha ya watu au ukaharibu maisha ya watu. Safiri salama, umebeba taifa la watanzania.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents