Burudani

Hizi ni nyimbo 2 ambazo Chemical angetamani kushiriki kwenye remix zake

Rapper Chemical amezitaja nyimbo mbili za Bongo Fleva ambazo anatamani awepo endapo zitakuwa na mipango ya kufanyiwa remix.

Hitmaker huyo wa ‘Mary Mary’ amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Muziki ya Darassa pamoja na Sisikii ya Maua Sama.

“Kuna ‘Muziki’ ya Darassa alimshirikisha Ben Pol ni wimbo ambao angefanya remix na mimi ningependa niwepo nafikiria ungefanya vizuri. Lakini pia wimbo mwingine ni ‘Sisikii’ wa Maua Sama,” amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One.

Chemical ameongeza kuwa anajitahidi kwenye kuflow pamoja na kuandika ili ifike kipindi watu wasimshindanishe kama rapper wa kike bali wamuone ni kama rapper anayefanya vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents